Nyota wa Bongo Fleva Diamond Platnumz ameacha kitendawili katika mitandao ya kijamii baada ya kuposti kuwa mjengo mrefu wa Wasafi umefikia asilimia 80 hivyo bado asilimia 20 tu.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter Diamond ameandika “WASAFI TOWER….80%”
Hata hivyo hakutoa maelezo Zaidi katika posti hiyo jambo ambalo limeibua mjadala watu wakitaka kujua mjengo huo unajengwa wapi na utakuwaje.