Leo May 6, 2020 Mwimbaji staa wa Bongofleva Harmonize ameonesha kumkumbuka na hata kuingia huruma juu ya ukimya wa mwimbaji Rich Mavoko ambaye amekuwa kimya kwa muda mrefu.
Rich Mavoko amekuwa kimya na hajapost kitu chochote toka January 1 mwaka huu na hajatoa kazi mpya toka alipoachia wimbo wake wa mwisho wa Babilon alioutoa miezi Nane iliyopita.
Sasa Harmonize ameandika haya kwenye ukurasa wake wa Instagram kuhusu Mavoko…
..”Familia Ngapi Zipo Nyuma Ya @richmavoko..?? Na zinamtegemea Yeye KwaKila Jambo Hasa Hili La Kupata Mkate Wa Kilasiku VP Kuhusu Ndoto Za Familia Hizo Na Zinaishije Katikwa Wakati Huu…???
. Ndoto Ngapi Za Wasani Ambao Wanategemea Kuzifikia Hizo Ndoto Kupitia Mavoco ..?? Na Nyuma Ya Hao Wasanii Kuna Familia NyenginePia ..??
.
Jeee Maumivu Malala Miko Ya Wazazi Wake Hasa Mama Mzazi Ambae Ndio Kama Roho Yake …!!! Ushajiuliza Ni Kauli Ngapi Za Uchungu Anazitoa Ambazo Zinaweza Kumpata Kila Anaefurahishwa Na Hili Kwa Makusudi ..???
.
Mana Mzazi wa Mwenzio Ni wako Pia Laana Yake Haishindwi Kukupata …!! La Mwisho Kabisa Mgeukie Mwenzio Anaefurahia Na Kuifanya Hii Kuwa Ni Habari Njema Kwake Ya Kumfanya Atembee Kifua Mbele Na Hata Kuandika Mtandaoni Kwa Furaha MAVOCO KAPOTEA muulize Anafaidika Nanini …???
.
Mungu Anasababu Na Maana Yake Bro @richimavocoKama Mdogoako Nakuombea Najua Ukimya Wako Unamaana Kubwa Sanaa Ndani Yako Ninachojua Ni Kujiweka Sawa Na Kutuletea Kazi Zingine Tunakupenda Na Tunakuombea Mungu Akufanyie Wepesi…!!! Let’s Go Bro Mdogoako Rafiki Yako Nipo Hapa Muda Wowote…!!!! RAMADAN KAREEM“ – Harmonize