MASUMBWI: Tyson Furry amtwanga mtu KO nchini Marekani, Mwenyewe amtangazia kiama mbabe Deontay Wilder
Mchezo huo usiokuwa wa ubingwa umepigwa katika ukumbi wa MGM Grand, Las Vegas, Marekani ambapo Tyson alimpiga KO mbabe huyo kunako raundi ya pili ya pambano hilo lililokuwa na raundi 12.
Kabla ya kupoteza pambano la leo, Shwarz alikuwa na rekodi ya kushinda mapambano yote aliyowahi kushiriki, ameshinda 24 (KO 16).
Baada ya pambano hilo, Tyson Furry amethibitisha kuwa mwezi Oktoba watarudia pambano na mbabe Deontay Wilder huku akimchimba mkwara mzito.
“Nitarudi tena Marekani, nafikiri itakuwa ni New York nakuja kupambana tena na Dentay Wilder na sio kupambana nakuja kumgaragaza,“amesema Tyson Furry kwenye mahojiano yake na kituo cha runinga cha ESPN.
Kwenye pambano la kwanza lisilo la ubingwa, lililopigwa mwezi Machi mwaka huu, Tyson Furry alitoka sare na Deontay Wilder.
Leave a Comment