Mwanamke Andrea Ivanova mwenye miaka 22 kutokea nchini Bulgaria, amesema ameongeza lips za mdomo wake ambapo siku ya Aprili 28, amechomwa sindano 20 za Asidi ya Hyaluronic ili kuongeza lips hizo.
Mwanamke huyo ambaye ni mwanafunzi wa falsafa “Philosophy” amekuwa ni mmoja kati ya watu wenye lips kubwa duniani, amesema ataendelea kuongeza lips zake mpaka pale atakapo ridhika.
Akizungumzia suala hilo la kuongeza lips zake amesema “Nazipenda sana lips zangu, nilipata ugumu kwenye kula kwa siku mbili hadi tatu baada ya kuchomwa sindano ila sasa hivi sipati ikwazo vyovyote, madaktari wamesema inatosha ila mimi nataka kubwa zaidi ila itabidi nisubiri angalau kwa miezi miwili”.
Andrea Ivanova amesema alianza kufanya mabadiliko ya lips za mdomo wake mwaka 2018, na anatumia Tsh 386,258 kwa kila matibabu, hadi hakumbuki jumla ya gharama zote alizotumia kwenye lips zake.