La Liga Wataka Mechi Kati Ya Barcelona – Real Madrid Kuahirishwa
Kumekuwepo na maandamano mjini Barcelona baada ya wanaharakati tisa wanaopigania kujitenga kwa Catalan kufungwa jela siku ya Jumatatu.
La Liga iliwasilisha ombi hilo kwa serikali ya Uhispania na klabu zote mbili zitaulizwa maono yao.
Awali BBC Sports inaelewa kwamba Barcelona ingekataa ombi hilo kwa kuwa klabu hiyo inaona ombi hilo la kuhamishwa halihitajiki.
Maandamano zaidi yanatarajiwa katika mji huo katika siku ya mechi hiyo na shirika la marefa linasema kwamba hatua hiyo inajiri katika mazingira yasioweza kuepukika.
Kamati ya ushindani katika shirikisho hilo inatarajiwa kufanya uamuzi wake katika siku chache zijazo.
Barcelona na Real Madrid hazikuhusishwa katika ombi hilo la La Liga na kwamba hakujakuwa na tamko lolote rasmi kutoka kwa klabu zote mbili.
Inamaanisha kwamba mechi hiyo iliyotarajiwa kuchezwa mwezi Machi sasa itafanyika mjini Barcelona.
Leave a Comment