Ukipenda Chips, Usiogope Mimba na Misemo Mingine ya Kuvunja Mbavu Kwenye Malori
Iwapo umekuwa ukisafiri kwenye barabara za nchini Tanzania, bila shaka umekutana na nukuu zilizoandikwa kwenye malori, mabasi na hata pikipiki
Misemo hiyo ya kuvunja mbavu mara nyingi huwa imeandikwa nyuma ya magari au hata ndani
Mara nyingi misemo hiyo mbali na kuwa ya kuibua uchesi huelezea tu hali halisi ya jinsi maisha yalivyo katika ulimwengu wa kisasa
1. Ukikosa tumaini kula tu matumbo
2. Maisha ni yangu matanga ni yenu
3. Waliokudharau siku moja watakudharau tena usipojikaza
4. Machozi ya nini na viboko bado
5. Kijiji kidogo umbea milioni
6. Punda haku soma lakini hakosi kazi
7. Utamu wa ugali ni aina ya mboga
8. Ukipenda chips, usiogope mimba

TUNAOMBA TUANDIKIE AU COMMENT MSEMO ULIOWAHI KUUONA NA WEWE HAPO CHINI KWENYE COMMENT
#Odinga#mitano#kenya
Eti ninamimbayako hukuzamanmi nishazaliwa
Kama hunpendi upo sawa maanami mwenyewe sijipendi
palipo na mungu na shetani yupo
Ukinisema sana angalia na yako usije kusahau
Ugumu wa vita usikufanye utupe silaha
Ukinipenda mm usisahau kujipenda mwenyewe
Ukikubali kuolewa sharti ulale,,,, nguo
hahahahahah